Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malengo ya SDGs hayotofanikiwa tusipotokomeza ubaguzi: Sidibe

UN Photo/Abel Kavanagh
Ishara ya kutokomeza ubaguzi wa rangi.

Malengo ya SDGs hayotofanikiwa tusipotokomeza ubaguzi: Sidibe

Haki za binadamu

Azima ya kuhakikisha afya kwa wote au malengo ya maendeleo endelevu SDGs havitoweza kufikiwa endapo dunia haitoukabili na kuutokomeza ubaguzi. 

Kauli hiyo imetolewa na Michel Sidibe mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya ukimwi UNADS katika kuelekea siku ya kimataifa ya kupinga ubaguzi ambayo kila mwaka huadhimishwa Machi Mosi.  

Mwaka huu katika siku hiyo kwa UNAIDS inajikita katika kuainisha haki ya kila mtu kuishi bila kubaguliwa kwa sababu ya ama umri wake, jinsia, mahusiano yake ya kimapenzi, ulemavu, rangi, kabila, lugha, hali ya kiafya kama kuishi na HIV au VVU, mahali atokako, hali yake ya kiuchumi, hali ya uhamiaji au sababu nyingine yoyote.

Hata hivyo shirika hilo linasema kwa bahati mbaya ubaguzi unaendelea kuathiri jitihada za kuwa na dunia yenye haki sawa, kwani mamilioni ya watu wanakabiliwa na ubaguzi kila uchao.

Sidibe ameongeza kuwa Kila mtu ana haki ya kuheshimiwa, kuishi huru bila kubaguliwa na  kukabiliwa na ukatili, kwani ubaguzi hauathiri mtu mmoja tu bali unaathiri kila mtu na kwamba

(SAUTI YA MICHEL SIDIBE)

Takwimu kutoka nchi 50 zinaonyesha kuwa mtu mmoja kati ya 8 wanaoishi na HIVwameripotiwa kukataliwa huduma za afya.”

Ametoa wito kwa kila mtu kuchukua hatua ya  kuzungumzia na kupinga hali hiyo.