Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada ya kujikwamua ni muhimu zaidi kwa wakimbizi Chad

Wakimbizi wa ndani nchini Chad. Picha ya OCHA/Mayanne Munan

Misaada ya kujikwamua ni muhimu zaidi kwa wakimbizi Chad

Haki za binadamu

Naibu Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na  usaidizi wa majanga, OCHA, Ursula Mueller amehitimisha ziara yake huko Chad iliyolenga kujionea hali halisi ya athari za mashambulizi yanayofanywa na Boko Haram. 

Burudani hii mahsusi kutoka kwa waendesha farasi wakimlaki Bi. Mueller kwenye uwanja wa ndege wa Bol nchini Chad, ikiwa ni ziara yake hapa baada ya kuhitimisha ziara kama hii huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na Cameroon.

Kisha mazugumzo na wakimbizi wa ndani wake kwa waume, kwenye kambi ya Yakoua, ambao wamesaka hifadhi kunusuru maisha yao dhidi ya ukatili wa Boko Haram.

Huyu anasema hawana ardhi, na fedha wanazopata ni kidogo.. Bi Mueller akafunguka..

(Sauti ya Ursula Mueller)

“Tuko hapa karibu na Ziwa Chad eneo ambalo lina rutuba sana. Kwa hiyo ni muhimu kusonga mbele badala ya kutoa misaada ya kibinadamu, tuwapatie ile ya kujikwamua ili watu waweze kuanza kujenga upya maisha yao. Tunaomba serikali ije na suluhisho la kudumu la usaidizi kwa kuwa bado wako hapa. Na kwa jamii ya kimataifa msaada wa kimaendeleo na kuwapatia boti na nyavu ili wavue samaki na wajilishe.”

Kambi ya ndani ya Yakoua inahifadhi wakimbizi wapatao 137,000.