Lebanon yasaidia UNIFIL -Lacroix

27 Februari 2018

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix amekamilisha awamu ya kwanza ya ziara yake katika eneo la Mashariki ya Kati.

Wakati wa ziara hiyo nchini Lebanon alikutana na viongozi waandamizi akiwemo Rais wa nchi hiyo pamoja na walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNIFIL, kikosi ambacho ndicho kikosi pekee cha Umoja wa Mataifa cha wanamaji.

Bwana Lacroix ameshukuru msaada pamoja na ushirikiano kutoka serikali ya Lebanon katika utekelezaji wa shughuli za UNIFIL.

Pia ameziopmba pande husika  kushirikiana kuendeleza ushwari uliokuwepo kwa muda wa miaka 11 katika eneo la kusini mwa Lebanon na kutafuta njia za kupata usitishwaji wa kudumu wa mvutano kati ya Lebanon na Israel.

Kikosi cha UNIFIL kiko kusini mwa Lebanon kwenye mpaka kati ya nchi hiyo na Israel na lengo ni kushika doria kuona harakati za kijeshi kati ya vikosi vya serikali ya Israel na  wapiganaji wa Hezbollah.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud