Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Homa ya Lassa ‘yarindima’ Nigeria-WHO

Wahudumu wa afya katika kambi ya wakimbizi wa ndani Nigeria. Picha: WHO

Homa ya Lassa ‘yarindima’ Nigeria-WHO

Afya

Watu 90 wanasemekana ndio wamefariki kutokana na homa ya Lassa  iliyolipuka mapema mwaka huu nchini Nigeria.

Shirika la Afya dunian WHO limesema leo kuwa idadi mpya ya waathirika wa homa ya Lassa ambayo imetolewa na  kituo cha kudhibiti magonjwa cha Nigeria-NCDC- inaonyesha kuwa kati ya Januari mosi na februari 25 mwaka 2018 visa 1,081 vya homa ya Lassa viliripotiwa ambapo 317  kati ya hivyo vilihakikishwa na maabara .

Msemaji wa WHO, Tarik Jasarevic, amewambia wandishi habari mjini Geneva kuwa idadi ya kesi zilizohakikishiwa  kwa kipindi cha wiki nane ni zaidi ya 305 idadi ambayo hadi sasa ndiyo kubwa kabisa kutokana na mlipuko wa homa ya

Lassa na kwamba

(SAUTI YA TARIK)

“Vifo 90 vimeripotiwa na 64 kati ya hivyo kuthibitishwa maabara na homa ya Lassa imekuwa inazikumba nchi za Afrika Magharibi ikiwemo Benini, Liberia na Sierra Leone, zote zimeripoti kuthibitishwa kwa homa hiyo mwezi uliopita.”

Homa ya Lassa inasababishwa na kirusi ambacho kinaamuambukiza mwanadamu kupitia chakula ama vyombo vya nyumbani viliyojaa mkojo na pamoja na kinyesi cha panya.

Dalili za ugonjwa huo ni homa kwanza, mtu hujisikia myonge, baada ya siku chache mgonjwa huanza kuumwa na kichwa, koo linalowasha, kuumwa na kifua, kutapika, kuharisha, na kusokotwa na tumbo, uso wa mgonjwa  unaweza kufura, kuumwa na mapafu na kutokwa damu mdomoni.

Homa hiyo hukaa mwilini kati ya siku 6 na 21.