Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila hatua za haraka tatizo la njaa Sudan kusini ni janga lisilo kwepeka: FAO

Raia wa Shilluk mkoani Wau wasajiliwa kwa ajili ya misaada ya kibinadamu. Picha: IOM/Sudan Kusini

Bila hatua za haraka tatizo la njaa Sudan kusini ni janga lisilo kwepeka: FAO

Haki za binadamu

Ripoti ya shirika la chakula na kilimo duniani FAO iliyotolewa leo imebaini kuwa zaidi ya watu milioni 7 wako hatarini kukabiliwa  na janga  la njaa  ambalo halijawahi kutokea katika siku za usonii, nchini Sudan kusini. Hivyo msaada wahitajika haraka  ili kuokoa maisha ya wengi. Selina Jerobon na tarifa kamili

Ripoti, hiyo inasema tangu mwezi Januari mwaka huu idadi ya watu takriban milioni 5.3 tayari wanakabiliwa na ukosefu wa chakula, katika maeneo mengi yalioko katika machafuko ikiwa ni asilimia 40 ya raia wote waishio nchini Sudan kusini.

Bwana Serge Tissot ambaye ni mwakilishi wa FAO Sudan kusini amesema hali ni tete nchini humo na bila kuwepo mikakati ya kusaidia, tatizo la njaa litazidi kuongezeka na raia wengi wataathirika.

Ameongeza kuwa njia ya kuongeza uhakika wa chakula ni pamoja na kuchukua hatua ya kuwawezesha wakulima kwa kuwapa mbinu za kuboresha kilimo haraka ili waweze kuzalisha mazao yatakayoimarisha hali ya uhakika wa chakula kutokana na ongezeko la uzalishaji .

Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo FAO, la kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula duniani WFP yamesema bila kuwepo na mikakati sahihi na ya haraka , tatizo la njaa Sudan Kusini, linaweza kurudisha nyuma hatua zilizopigwa dhidi ya tatizo la  njaa nchini kumo na ukanda mzima wa Afrika ya kati.