Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Je unawezaje kumudu saratani ukiwa ukimbizini bila fedha?

Baadhi ya wakimbizi wa kabila la Rohingya . (Picha:UM/IOM)

Je unawezaje kumudu saratani ukiwa ukimbizini bila fedha?

Haki za binadamu

Hali ya kuwa mkimbizi ni mtihani tosha, ukiongeza changamoto za kiafya kama saratani , ambapo hata huduma za afya huwezi kumudu  inakuwaje? 

Ile kuambiwa una saratani hata kama sio mkimbizi inatisha na kukatisha tamaa, sasa kwa mkimbizi ambaye anategemea msaada kwa kila kitu mtihani ni mara mbili, na hayo ndio yaliyomfika Mohammad mwenye umri wa miaka 60, mkimbizi kutoka Myanmar aliyefungasha virago na mkewe Julekha baada ya machafuko ya Rohingya kushika kasi miezi sita iliyopita.

Amekuwa akisumbuliwa na tumbo tangu Myanmar na walipowasili kambini Bangladesh baada ya madhila mengi njiani  akawa taabani kama anavyosimulia mkewe

(JULEKHA CUT 1)

“Kulikuwa na mashambulizi ya risasi, kila kitu kilichotuzunguka kiliteketea kwa moto, tulipata hifadhi katika Kijiji cha jirani kwa wiki tatu. Ikatulazimu kukimbia tena, na kutembea kwa siku 8 tukivuka mito huku mvua ikinyesha kutwa.”

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM , Mohammad alijaribu kila dawa Bangladesh bila mafanikio, na ndipo alipopelekwa kwenye hospitali ya taifa na kuambiwa kuwa na saratani ya tumbo. Kiasi kidogo cha fedha walichokuwa nacho kikaisha ikabidi aondeke bila hata kuanza tiba

(JULEKHA CUT 2)

“IIlibiti tutumie taka 35,000 sawa na dola 420, tukapoteza matumaini, watu wakatuambia atakufa.”

Na baada ya kiza totoro nuru ikaanza kuangaza, familia ilipobaini kituo cha afya cha IOM kambini, alipowasili kwa msaad wa IOM walimuhamishia hispitali ya taifa kwenda kupata huduma ya bure

(JULEKHA CUT 3)

“Tuna furaha , tuna furaha sana kuweza kufika hapa bila hata kuhitaji fedha, kwa neema ya mungu tutapata matibabu bure kila siku, watoto wetu wanasema atapata nafuu. Tuna furahja sana nani ambaye hawezi kufurahia hili.”

Ingawa Mohammad bado ana changamoto nyingi za kiafya, tayari ameshafanyiwa upasuaji na familia yake ina matumaini  kwa sasa, asante kwa IOM.