Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Azimio kuhusu Ghouta Mashariki litekelezwe- Guterres

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lapitisha azimio la sitisho la mapigano huko Syria
UN Photo/Manuel Elías
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lapitisha azimio la sitisho la mapigano huko Syria

Azimio kuhusu Ghouta Mashariki litekelezwe- Guterres

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amefungua kikao cha 37 cha Baraza la Haki za Binadamu la umoja huo huko Geneva, Uswisi akitaka utekelezaji wa haraka wa sitisho la mapigano huko Syria baada ya Baraza la Usalama kupitisha kwa kauli moja azimio hilo.

Katibu Mkuu amesema azimio hilo linataka sitisho la mapigano kwa siku 30 lakini..

(Sauti ya Antonio Guterres)

“Maazimio ya Baraza la Usalama yanakuwa na maana iwapo yanatekelezwa kwa ufanisi. Na ndio maana natarajia azimio hilo litekelezwe haraka na lizingatiwa hasa katika kuhakikisha huduma na misaada ya kibinadamu inafikishwa bila vikwazo, wagonjwa wahamishwe ili kupunguza machungu ya wasyria.”

Akiangazia tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linalotimiza miaka 70 mwaka huu, Katibu Mkuu amesema ingawa kuna mafanikio ya uzingatiaji wa haki bado haki za binadamu zinasiginwa..

(Sauti ya Antonio Guterres)

“Lakini ni dhahiri kuwa maneno yaliyomo kwenye tamko hilo bado hayaendani na hali yalisi mashinani. Kivitendo, watu kote ulimwenguni bado wanakumbwa na vikwazo au hata wananyimwa haki zao za msingi. Usawa wa kijinsia unasalia hoja nzito, idadi ya wanawake na wasichana isiyofahamika wakikumbwa na ukosefu wa usalama, ghasia na haki zao kukiukwa.”

Amesema ni vyema kutambua kuwa haki za binadamu si anasa bali ni ni bali ni wajibu ulioridhiwa na nchi wanachama.

Naye Kamishna Mkuu  wa haki za binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein ametumia jukwaa hilo kuwanyooshea vidole wakiukaji wa haki akisema..

(Sauti ya Zeid Ra’ad Al Hussein)

“Hakuna tamadunia, sheria au dini inayounga mkono ukandamizaji. Mijadala kuhusu haki inaepukwa na wale wanaosaka kuipindisha kwa sababu ya kuhisi lawama, wale ambao wanaona aibu kuchukua uamuzi mgumu na wanufaika wa chambuzi zisizo na mashiko.”