Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunasaka misaada endelevu badala ya dharura pekee- UNHCR

Wakimbizi wapya waliowasili kituo cha dharura cha UNHCR huko Sebagoro nchini Uganda tarehe 11 mwezi Februari mwaka 2018 kutoka DRC.
UNHCR/Michele Sibiloni
Wakimbizi wapya waliowasili kituo cha dharura cha UNHCR huko Sebagoro nchini Uganda tarehe 11 mwezi Februari mwaka 2018 kutoka DRC.

Tunasaka misaada endelevu badala ya dharura pekee- UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

Wakimbizi wanapowasili ugenini huduma ya kwanza ni mahitaji ya dharura kama vile maji, huduma  za afya na malazi kinachofuatia ni huduma za baadaye na endelevu. Mahitaji kama vile stadi za kazi na hata ajira.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Uganda limesema limechukua hatua kuhakikisha  ili kuwapatia wakimbizi nchini humo misaada ya endelevu badala ya ya ile ya dharura pekee.

Joyce Munyao Mbithi,ambaye ni afisa mwandamizi wa uhusiano wa UNHCR nchini Uganda amesema hayo kufuatia ziara ya maafisa waandamizi wa shirika hilo pamoja wa wafadhili kwenye makazi ya wakimbizi ya Kyaka II kilometa 200 kutoka mji mkuu Kampala.

Bi. Munyao-Mbithi amesema..

(Sauti ya Joyce Munyao-Mbithi)

Kwa mantiki hiyo amesema mwelekeo ni..

(Sauti ya Joyce Munyao-Mbithi)

Kwa mujibu wa UNHCR, Uganda ina mfumo wa aina yake wa kusaidia wakimbizi ambapo raia hao hupatiwa ardhi kwa ajili ya kujenga makazi pamoja na shughuli za kilimo.