Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wa Rohingya 720,000 mashakani-UNICEF

© UNHCR / Andrew McConnell
Watoto waRohingya katika kambi ya Chonkhola huko Chakdhala, Bangladesh.

Watoto wa Rohingya 720,000 mashakani-UNICEF

Msaada wa Kibinadamu

Msimu wa mvua na pepo kali unaokaribia pamoja na ghasia kwa upande mwingine ni mwiba kwa watoto zaidi ya 700,000 waliokumbwa katika mgogoro wa wakimbizi wa Rohingya.

Mkurugenzi wa UNICEF anayehusika na miradi ya dharura, Manuel Fontaine,amesema kuwa takriban watoto 720,000 ni kama wamezingirwa au wako makazi ya muda  ya kulazimishiwa huko Myanmar au wanaishi kwenye kambi zilizojaa pomoni nchini Bangladesh kwa sababu hawawezi kurudi makwao. Akihofia athari za msimu huo wa mvua  Viviane van Steirteghem mkuu wa ofisi ya UNICEF Cox Bazar

(SAUTI YA VIVIANE VAN STEIRTEGHEM)

“Tuna msimu wa mvua unakuja na tuna mengi ya kujiandaa , tunajua baadhi ya watu vado wanaishi katika maeneo ya mwinuko milimani na kunaweza kuwa na maporomoko , na tunafahamu kwamba watu wengi wanaishi katika maeneo ambayo yatafurika kabisa.”

Ameongeza kuwa kambi za wakimbizi pia huenda zikaathirika na hivyo

( SAUTI YA VIVIANE VAN STEIRTEGHEM)

“Fursa ya huduma za afya, elimu, ulinzi wa watoto vitatoweka, na hata fursa ya maji safi na usafi , tunahitaji kuliangalia kwa makini hili kwa sababu viko hatarini.”

Ripoti hiyo inatolewa wakati ni miezi sita tangu warohingya waanze upya kukimbilia kusini mwa Bangladeshi wakitokea Myanmar.

Ripoti inaendelea kueleza kuwa takriban watoto 185,000 bado wamekwamia katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar ambako waliachwa na wazazi wao waliotoroka ghasia.