Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna madai 40 ya ukatili na unyanysaji wa kingono UN inayafanyia kazi

Stephane Dujarric, msemaji wa Umoja wa Mataifa akizungumza na waandishi wa habari.
UN /Manuel Elias
Stephane Dujarric, msemaji wa Umoja wa Mataifa akizungumza na waandishi wa habari.

Kuna madai 40 ya ukatili na unyanysaji wa kingono UN inayafanyia kazi

Haki za binadamu

Umoja wa Mataifa  umesema utaendelea kufuatilia na kuchukua hatua huku ukiyafanyia kazi madai yote ya unyanyasaji na ukatili wa kingono kwenye mfumo wa Umoja wa mataifa kwa kuzingatia mkakati wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa uwazi dhidi ya madai hayo.

Hayo yameelezwa na msemaji wa Umoja wa Mataifa hii leo Stephane Dujarric akizungumza na waandishi wa Habari mjini New York Marekani  na kuongeza kuwa tangu Oktoba Mosi hadi Desemba 31 mwaka 2017 Umoja wa Mataifa umepokea madai 40 dhidi ya mashirika yake na watendaji wadau, ingawa amesema siyo madai yote yaliyothibitishwa na mengi bado yako katika hatua za mwanzo za tathimini na kwamba

(SAUTI YA STEPHANE DUJARRIC )

Kati ya Madai hayo 40, Madai 15 yameripotiwa kutoka kwenye operesheni za ulinzi wa amani na yote yameingizwa katika orodha ya maadili na nidhamu kadri yalivyokuwa yakija, yaliyosalia 25 yameripotiwa kutoka mashirika, mifuko na programu , yakiwemo madai 8 yanayohusiana na watendaji wadau.”

Ameongeza kuwa kati ya madai hayo 40 , madai 13 yatajwa kuwa ni ya ukatili wa kingono, 24 ya unyanyasaji wa kingono na matatu hayajulikani ni ya nini na kwamba

(SAUTI YA STEPHANE DIJARRIC)

“Madai hayo 40 yanajumuisha waathirika 54, wakiwemo 30 wanawake, 16 wasichana wa chini ya umri wa miaka 18 na umri wa waathirika 8 haujulikani. Madai 12 kati ya hayo 40 yaliyalifanyika mwaka 2017, madai 7 mwaka 2016, madai 3 mwaka 2015 au kabla ya hapo na tarehe za madai 18 hazijulikani.”

Amesema hadi sasa madai mawili kati ya 40 yameshathibitishwa na uchunguzi, 3 hayajathibitishwa, 15 yako katika hatua mbalimbali za uchunguzi, 18 yako katika hatua za awali za tathimini na 2 yanafanyiwa tathimini kukiwa na taarifa chache zilizokabidhiwa kwa wachunguzi.

Kwa Umoja wa Mataifa ambao una walinda amani 90,000 na wafanyakazi raia zaidi ya 95,000, Dujarric amesema unyanyasaji na ukatili wa kingono sio sehemu kubwa ya wanawake na wanaume wanaohudumu katika shirika hilo, akisisitiza kwamba hata hivyo kila dai dhidi ya mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa linaweka hatarini maadaili, misingi na kujitolea kunakofanywa na wafanyakazi wengine wanaojitoa kimasomaso na kuzingatia maadili katika sehemu mbalimbali duniani.

Na kwa mantiki hiyo kukomesha uhalifu huo, na kuwawezesha waathirika kutaendelea kuwa kipaumbele cha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2018.

Wakati hayo yakiendelea ,mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudmia watoto UNICEF Harietta Fore leo ameekubali kujiuzulu kwa naibu mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Justin Forsyth, na kumshukuru kwa kazi yake kubwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita ya kuokoa Maisha ya watoto kote duniani kupitia wadhifa wake.