Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu kwangu ni ufunguo wa maisha- Nousa

Elimu ni mojawapo ya haki za watoto. Picha ya UNICEF Tanzania / Robin Baptista

Elimu kwangu ni ufunguo wa maisha- Nousa

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Nchini Misri, msichana mkimbizi kutoka nchini Sudan ameanza kuona nuru katika maisha yake baada ya kupata fursa ya kupata elimu nchini humo. Patrick Newman na ripoti kamili.

(Taarifa ya Patrick Newman)

Nats

Nousa Noussa Saber Sleiman, msichana  kutoka Sudan alihamia Misri kama mkimbizi miaka 3 iliyopita akiwa na lengo la kutafuta elimu ili aweze kujikwamua kimaisha yeye na nduguze.

Kama ilivyo kwa wakimbizi wengine kutoka Sudan, Noussa alipata fursa ya kusoma katika shule ya kikatoliki ambayo kwa msaada wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, hutoa elimu kwa zaidi ya wakimbi 400 wa asili ya Sudan mjini Cairo, Misri.

(Sauti ya Noussa Saber Sleiman)

“Elimu ni kila kitu katika maisha ya leo. Cha msingi kwangu ni kusoma kwa bidii ili niweze kuwasaidia ndugu zangu na pia kuwa mfano bora kwa wadogo zangu.”

Serikali ya Misri inaruhusu wakimbizi kupata elimu bure kama ilivyo kwa wazawa katika shule za serikali. Noussa ni miongoni mwao..

(Sauti ya Noussa Saber Sleiman)

“Tulipoondoka Sudani, tulipitia  matatizo mengi sana na hakuna aliyetusaidia.” 

Nchini Misri kuna zaidi ya  wakimbizi laki mbili kutoka mataifa 56 duniani ambapo asilimia 40 wametoka Syria na Sudan pekee.