Licha ya vikwazo vya usalama kampeni ya chanjo lazima isonge mbele- WHO
Shirika la Afya ulimwenguni WHO, limesema pamoja na kuwa linakabiliwa na tatizo la usalama bado linaendeleza kampeni ya chanjo Sudan kusini, hususani katika maeneo Jonglei na ukanda wa mto Nile ili kupunguza kusambaa kwa magonjwa ya donda koo na mengine.
Bwana Kofi Boeteng ambaye ni mtaalamu wa kampeni za chanjo wa WHO amesema japo wamepiga hatua kubwa katika kutoa chanjo kutoka asilimia 45 mwaka 2016 mpaka asilimia 56 mwaka jana bado kuna changamoto kubwa kuwafikia wananchi katika maeneo yalioko chini ya utawala wa wanamgambo ambao ni asilimia kubwa.
Mtaalamu huyo pia anatilia mkazo suala la kuwapata wataalam uwa afya wenye uzoefu ili kuweza kutoa huduma bora na yenye tija kwa wananchi ambao ndio walengwa wakubwa, na waliokwama katika sehemu mbalimbali isiyokuwa na huduma yenye kukidhi mahitaji muhimu ya afya.
WHO imesema changamoto kubwa wanalokabiliana nalo kutowafikia wananchi walio wengi nchini Sudan kusini wakati wa kutoa chanjo ni pamoja na ushirikiano mdogo kutoka kwa vyongozi wa apande zote, miundombinu, ukosefu wa wataalamu na pia ukosefu wa takwimu sahihi za wananchi kutokana na hali ya usalama katika baadhi ya maeneo ambayo hayafikiki.