Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za binadamu na usalama bado kitendawili CAR

Kinamama na watoto wakimbizi wa ndani katika kituo kimoja mjini Paoua, CAR
Yaye Nabo Sène/OCHA
Kinamama na watoto wakimbizi wa ndani katika kituo kimoja mjini Paoua, CAR

Haki za binadamu na usalama bado kitendawili CAR

Haki za binadamu

Mtaalam huru wa haki za kibinadamu wa Umoja wa mataifa, Bi Marie Therese Bocum anatarajia kuanza ziara nchini jamhuri ya Afrika ya kati CAR  kuanzia tarehe 6 hadi 16 Machi  kwa lengo la kutathmini hali ya utawala wa sheria na haki za kibinadamu nchini humo.

Katika ziara hiyo Bi Therese atakutana na viongozi wa serikali, viongozi wa dini, mashirika ya kibinadamu na asasi za kiraia ili kujadili utawala wa shera na pia utekezaji wa haki za binadamu katika taifa hilo lililoghubikwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na pia vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu.

Bi Therese amesema , anasikitika kwamba baadhi ya makundi ya upinzani yalioalikwa kwenye meza ya mazungumuzo kama kundi la ukombozi wa Afrika ya kati MNLC, Umoja wa amani Afika ya kati UPC na makundi mengine ya vyama vya upizani na  wanamgambo bado wanaendelea kutia vikwazo katika mchakato wa kusaka  mwafaka wa amani ya taifa hilo, chini ya usimamizi  wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini CAR, MINUSCA.

Maalumu huyo  anatoa wito kwa viongozi wa serikali, jamii ya kimataifa na  pande zote kizani kunzingatia makubaliano ya amani ili kupata suluhu la kudumu katika mgororo huo uliosababisha maafa kwa raia, ukosefu wa huduma za afya, usalama na pia ukimbizi wa ndani na nje kwa mamiolini ya wananchi.