Lugha ya mama ni muaroabaini wa kufanikisha SDGs- UNESCO

21 Februari 2018

Uwepo wa lugha za mama tofauti duniani ni muhimu ili kuendeleza mizania badala ya kupatia kipaumbele lugha chache huku nyingine muhimu zikitoweshwa, amesema Dkt. Elifuraha Laltaika kutoka Tanzania, mtaalamu huru wa jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa asili alipozunguma na Idhaa ya Umoja wa Mataifa kuhusu siku ya lugha ya mama ulimwenguni  hii leo.

Kila wiki mbili zinapopita, lugha moja ya asili inayotumika duniani inatoweka! Amesema Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoaj wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni, UNESCO, Audrey Azoulay katika ujumbe wake wa siku ya lugha ya mama duniani hii leo. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

 (Taarifa ya Assumpta Massoi)

 Hawa ni watoto wamasai katika moja ya burudani zao kupitia lugha yao ya mama! UNESCO inasema  kuwa lugha ya mama ni msingi wa kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, kwani matumizi ya lugha ya mama yanawezesha mtu kupokea maarifa mapya kwa urahisi kuliko kupitia lugha ya mapokeo au lugha ya kigeni.

Ili kufahamu uhusiano huo, nimezungumza na Dkt. Elifuraha Laltaika kutoka Tanzania ambaye ni mtaalamu huru wa jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa asili nikamuuliza ni kwa vipi?

(Sauti ya Dkt. Elifuraha Laltaika)

UNESCO inasema kuwa lugha ni zaidi ya mawasiliano, hili nalo linathibitika vipi Dkt. Laltaika?

(Sauti ya Dkt. Elifuraha Laltaika)

Mahojiano kamili na Dkt. Laltaika ambaye pia ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira nchini Tanzania yatapatikana kwenye wavuti wetu www.news.un.org/sw

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter