Watu milioni 2.4 wanahitaji msaada Burundi 2018:OCHA

20 Februari 2018

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masaula ya dharura OCHA limezindua mjini Bujumbura Burundi mpango wa usaidizi wa kibinadamu nchini humo (HRP) kwa mwaka 2018.

Kwa mujibu wa shirika hilo watu milioni 2.4 wanahitaji msaada wa kibinadamu katika nchi nzima kwa mwaka huu ikiwa ni mara mbili ya idadi ya watu waliolengwa mwaka jana.

OCHA inasema kwa ujumla watu milioni 3.6 wanahitaji msaada wa aina moja au nyingine Burundi na zaidi ya robo ya raia wote wa nchi hiyo wanakadiriwa kutokuwa na uhakika wa chakula, idadi ambayo ni sawa na ongezeko la aslimia 7 ikilinganishwa na mwaka 2016.

Fedha zinazohitajika kutekeleza mpango huo (HRP) ni takribani dola milioni 142, na mpango utajikita zaidi katika kuwasaidia wakimbizi wa ndani wanaorejea makwao, kuwajumuisha katika jamii wakimbizi wanaorudi nyumbani, watu waliorejeshwa na pia kuwasaidia maelfu waliokumbwa na majanga ya asili.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter