Brazili iwe mfano wa kuwaenzi wakimbizi:Grandi
Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filipo Grandi amekutana na wawakilishi wa nchi 36 za Amerika ya kusini na visiwa vya karibea nchini Brazil, katika mkutano wa kimataifa kuhusu ulinzi wa wakimbizi ili kujadili maswala nyeti yanayowababili wakimbizi katika ukanda huo.
Katika mkutano huo wa kimataifa, Grandi, na wawakilishi hao wamefikia makakubaliano ya kushirikiana katika kutoa hifadhi ya kudumu na pia kutetea haki za watu wanaosaka hifadhi au kukimbia kachafuko nchini mwao ambapo amesema
Sauti ya Filipo Grandi
“Sinabudi kuishukuru serikali ya Brazil, kupitia waziri wa mambo ya nje kwa jitihada za kuandaa mkutano huu mihumu sana wa kikanda . Wakati umefika ambapo ni lazma kusimamia misingi ya utu kama ilivyo desturi ya Amerika ya kusini na visiwa vya Karibea. Wakati huo huo tukikumbushia ahadi ya Brazil katika kutoa kipaumbelekatika mkutano wa kimataifa kuhusu ulinzi wa wakimbizi.
Na kuhusu baadhi ya nchini za Amerika kusini na visiwa vya Karibea ambazo bado zinaonyesha dalili za kusuasua kufikia mwakafaka katika makubaliano ya kimataifa kuhusu ulinzi wa wakimbizi na wasaka hifadhi mkuu huyo wa UNHCR amesema….
Sauti ya Filipo Grandi
Natumai nchi zingine za Amkerika kusini na visiswa vya Karibea pia zitatengeneza sera nzuri kuhusu ulinzi na hifadhi ya kudumu kwa wakimbizi kama ilivyo toa mfano wa Brazil . Ushirikiano wa masuala ya uhamiaji baina ya baadhi ya visiwa vya Karibea na shirika la Umoja wa mataifa ya Uhamiaji IOM, ni hatua nzuri katika kukabili mapungufu yatokanao na sera mbaya ya uhamiaj katika baadhi ya nchi.