Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutana na mtawa anayebadili maisha ya maelfu ya wanawake DRC

Wanawake wanaohsikilia nafasi mbali mbali katika jamii,Afrika Mashariki.(Picha:UM)

Kutana na mtawa anayebadili maisha ya maelfu ya wanawake DRC

Wanawake

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC wanawake wanapitia madhila makubwa kutokana na vita vya muda mrefu vinavyoendelea na vilivyosababisha zahma ya kibinadamu ikiwaacha waathirika wakubwa ambao ni wanawake na watoto katika taharuki. Lakini mtawa mmoja , sista Angelique amedhamiria kufuta machozi yao.

Akiwa mitaani na baiskeli yake na dhamira ya ukombozi, sista Angelique anatambua kuwa maelfu ya wanawake wamekwepa kutekwa, kuteswa na unyanyasaji wa kingono na anataka kubadili fikra hizo na kuwapa matumaini

(Sauti ya Sista Angelique)

“Ninapowaona wanakuja toka msituni wakiwa wametawanywa na kukimbia zahma , nyuso zao zinaonekana tofauti kabisa.”

Sasa Sista Angelique anawasaidia wanawake hao manusura kujenga upya maisha yao kwa kuwafundusha kusoma na kuandika , na kwa kuwapa mafunzo hayo anawasaidia kujitegemea.

(Sauti ya Sista Angelique)

“Endapo nitaweza kumsaidia hata mwanamke mmoja tu kuanza upya Maisha yake kwangu mimi hayo tayari ni mafanikio, kamwe sintokata tamaa.”

Shirikala Umojawa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema Sista Angelique kwa kufanya hivyo anatuma ujumbe mzito kwamba wanawake ni wastahimilivu na wanaweza kukabili lolote.