Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

India kuwa mwenyeji wa siku ya mazingira duniani 2018: UNEP

Taka zilizopo kando ya bahari. Picha: UM

India kuwa mwenyeji wa siku ya mazingira duniani 2018: UNEP

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Leo waziri waziri wa mazingira, misitu na mabadiliko ya tabia nchi wa India, Dr. Harsh Vardhan, na Katibu mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP Erik Solheim, kwa pamoja mjini Delhi India,  wameitangaza India kuwa mwenyeji wa siku ya mazingira duniani kimataifa kwa mwaka huu.

Siku hiyo ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 5 June , mwaka huu 2018 imebeba kauli mbiu ya ”komesha uchafuzi wa mazingira utokanao na plastiki” ukizitaka serikali, viwanda, jamii na watu binafsi kuungana na kutafuta njia mbadala ambayo ni endelevu  na itakayopunguza haraka uzalishaji na matumizi ya kupindukia ya mara moja ya plastiki zinazochafua mazingira ya bahari , kuathiri viumbe wa majini na kutishia afya ya binadamu.

Akizungumzia heshima hiyo kubwa Dr. Harsh Vardhan. Amesema India ina historia ya muda mrefu ya kukumbatia maisha ya pamoja na maliasili na imejizatiti kuifanya dunia kuwa safi na yenye mazingira bora.

Naye mkuu wa UNEP Erik Solheim amesema India itakuwa mwenyeji mzuri wa kimataifa wa siku hiyo kwani imeonyesha uongozi bora katika kukabili mabadiliko ya tabia nchi na haja ya kuahamia kwenye uchumi utumiao kiwango kidogo cha hewa ukaa na sasa itakuwa mstari wambele katika kuchagiza ukomeshaji wa matumizi ya plastiki duniani.

Siku ya mazingira duniani ilianza kuadhimishwa mwaka 1972 na sasa imekuwa ni maadhimisho ya kimataifa yenye lengo la kuelimisha umma kuhusu mazuala mbalimbali yahusuyo mazingira.