Ajali ya ndege Iran, Guterres atuma rambirambi

18 Februari 2018

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa watu 66 wamefariki dunia kwenye ajali ya ndege hii leo huko Iran na tayari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma salamu za rambirambi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa  Mataifa Antonio Guterres ameelezea masikitiko yake kufuatia ajali ya ndege iliyotokea leo huko Iran na kusababisha vifo.

Vyombo vya habari vyaripoti kuwa watu 66 wamefariki dunia baada ya ndege hiyo abiria ya shirika la ndege la Asema kuanguka kwenye milima ya Zagros nchini Iran wakati ikiwa safarini kutoka mji mkuu Tehran kuelekea mji wa Yasuj ulioko kusini-mashariki mwa nchi hiyo.

Guterres kupitia taarifa ya msemaji wake ametuma salamu za rambirambi kwa familia za marehemu na serikali ya Iran.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter