Teodora yuko huru baada ya miaka 10 jela kwa mwanae kufia tumboni

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Uswisi.
UN Photo - Jean-Marc Ferre
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Uswisi.

Teodora yuko huru baada ya miaka 10 jela kwa mwanae kufia tumboni

Haki za binadamu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa  leo imekaribisha habari za serikali ya El Salvador  kumuachilia huru mama aliyehukumiwa miaka 30 jela kwa kudaiwa kumuua mwanaye pale alipojifungua kujifungua mtoto aliyekufa.

Teodora Vásquez ambaye hadi leo akiwa ameshatumikia kifungo hicho kwa miaka 10, ni mmoja wa wanawake wanene waliokutana na Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein alipozuru nchini humo mwezi Novemba mwaka jana.

Wanawake wote wanne walikuwa wamehukumiwa miaka 30 kwa makosa yanayohusiana na mauaji kwa sababu ya mimba kuharibika au matatizo mengine ya dharura za kiafya yaliyochangia kupoteza watoto kabla hawajazaliwa.

Wakati huo Zeid alisema hajawahi kuguswa kama jinsi alivyogusa na hadithi za kina mama hao na ukatili mkubwa walioupitia, na ndipo akatoa wito kwa  serikali kwamba kesi zote za wanawake wanaoshikiliwa kwa sababu ya sheria ya El Salvador ya kuzuia utoaji mimba kutathiminiwa upya na kuwatendea haki.