Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iran acheni kuwanyonga watoto mnakiuka sheria za kimataifa: Zeid

UN Photo - Jean-Marc Ferre
Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein akihutubia waandishi wa habari. Picha:

Iran acheni kuwanyonga watoto mnakiuka sheria za kimataifa: Zeid

Haki za binadamu

Kamisha Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein leo ameitaka serikali ya Iran kuheshimu, kuzinhatia sheria za kimataifa na kukomesha mara moja unyongaji wote wa watu waliohukumiwa kifo kwa makossa waliyoyatenda wakiwa watoto, barubaru au vijana wadogo.

Amesema katika mwezi wa kwanza wa mwaka huu 2018 , watu watatu wakiwemo wanaume wawili na mwanamke mmoja walinyongwa kwa makossa waliyotenda walipokuwa na umri wa miaka 15 au 16 ikilinganishwa na watu watano wa umri kama huo walionyongwa katika kipindi cha mwaka mzima wa 2017.

Zeid ameongeza anasikitika kusema kwamba, Iran inakiuka sheria za kimataifa mara nyingi zaidi kuliko taifa lingine lolote, kwa kutekeleza mauaji hayo yaliyopigwa marufuku chini ya sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Amesisitiza kuwa hakuna taifa lolote linalokaribia idadi ya vijana wadogo walionyongwa Iran katika miongo kadhaa iliyopita akionya  kwamba hali hiyo haikubaliki na haipaswi kuendelea.