Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yazindua mwongozo wa kupambana na viwavi jeshi Afrika

Mkulima katika shamba lake lililoshambuliwa na viwavi jeshi huko Namibia
FAO/Rachael Nandalenga
Mkulima katika shamba lake lililoshambuliwa na viwavi jeshi huko Namibia

FAO yazindua mwongozo wa kupambana na viwavi jeshi Afrika

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Leo shirika la chakula na kilimo FAO limezundua mwongozo wa kina wa kudhibiti wadudu hatari  kwa mahidi, viwavi jeshi katika barani Afrika. 

Mwongozo huo mahsusi kwa ajili ya shule za kilimo utawasaidia wakulima wadogowadogo na wafanyakazi wa sekta ya kilimo kudhibiti ipasavyo viwavi jeshi (FAW) wakati huu ambapo hofu imetanda kuwa viwavijeshi hivyo vitawatumbukiza watu wengi zaidi katika baa la njaa Afrika.

Maeneo yaliyoa katika tahadhari ya juu ni Katikati na Kusini mwa Afrika ambako msimu wa upanzi wa mahindi unaendelea. Mwongozo huo umesheheni ushauri, unatoa msaada kwa wakulima wa Afrika wanaokabiliwa na zahma hii na pia kuwapa njia mbadala zinayojumuisha mbinu mbalimbali, zinayojali mazingira na zilizo endelevu.

Shamba la mahindi lililoshambuliwa na viwavi jeshi Malawi
FAO/Rachel Nandalenga
Shamba la mahindi lililoshambuliwa na viwavi jeshi Malawi
Shamba la mahindi lililoshambuliwa na viwavi jeshi Malawi, by FAO/Rachel Nandalenga

Allan Hruska ni mratibu mkuu wa masuala ya kiufundi kuhusu viwavi jeshi katika idara ya FAo ya ulinzi wa mimea na uzalishaji, anaongeza

(SAUTI YA ALLAN HRUSKA)

“Mwongozo huu ni tarifa za kiufundi na njia za kutumia kupitia shule za kilimo ili kuwafikia mamilioni ya wakulima wadogowadogo, ili wawe na uelewa, uzoefu ujasiri wa kudhibiti zahma hii katika mashamba yao ya mahindi na kuchukua hatua itakayokuwa endelevu ambayo haitokuwa na gharama kubwa na athari ndogo sana kwao.”