Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yahamisha wakimbizi 150 kutoka Libya na kupelekwa Italia

Ndege iliyokombolewa IOM inasafirisha wahamiaji 155 wa Guinea, ikiwa ni pamoja na watoto 10 kurudi makwao. Hii ni ndege ya nne tangu Mapema Novemba. Picha: IOM

UNHCR yahamisha wakimbizi 150 kutoka Libya na kupelekwa Italia

Haki za binadamu

Wakimbizi 150 walio hatarini Libya leo wameshamishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kutoka nchini humo  hadi Italia.

Wakimbizi hao wakionekana kuwa na hamasa huku wakijiandaa kupanda ndege kwenda kuanza maisha mapya, UNHCR inasema idadi hiyo inafanya jumla ya wakimbizi walioahamishwa Libya la kulepekwa taifa la tatu kuliko na usalama kufikia zaidi ya 1000 tangu kuanza kwa opereshenni hiyo miezi mitatu iliyopita.

Idadi kubwa ni wanawake, watoto na vijana , na baada ya kuwasili Roma Italia Carlotta Sami, msemaji wa UNHCR anasema hatua hii ya kuwahamisha wakimbizi hao ni muhimu sana maana wengi wamekuwa wakishikilia  katika vituo Libya kwa muda mrefu.

(SAUTI YA CARLOTTA SAMI)


"Hawa ni wanawake, hawa ni watoto na vijana wakimbizi ambao tangu miaka michache iliyopita wamekuwa wanashikiliwa kwenye vituo katika mazingira ya hatari sana. Ni watu wasiojiweza na hii ni ndege ya tatu inayoturuhusu kuwahamisha wakimbizi hawa haraka kutoka Libya moja kwa moja hadi Italia tunaushukuru uongozi wa Italia, na kwa UNHCR cha muhimu zaidi  ni kupata maeneo mengine, au nchi nyingine kuonyesha utashi wa kuwapokea wakimbizi hawa walio katika hali ya hatari.”