Watoto hatarini sababu ya pengo la takwimu:UNICEF

15 Februari 2018

Mapengo kwenye takwimu za wakimbizi, wahamiaji na wakimbizi wa ndani yanaweka hatarini maisha na mustakhbali wa mamilioni ya watoto waliosafarini, yameonya leo mashirika matano ya Umoja wa Mataifa na wadau wake.

Mashirika hayo la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, la kuhudumia wakimbizi UNHCR, la uhamiaji IOM, Eurostat na OECD katika wito wao wa kuwalinda watoto yamesama ulinzi huo unaanza na tawkimu bora na sahihi, na yameonyesha ni jinsi gani takwimu zilivyo muhimu kwa kuelewa mwenendo wa uhamiaji wa kimataifa ili kuweza kuunda será za kusaidia makundi yaliyo hatarini kama watoto.

Wito huo wa “kuchukua hatua” unathibitisha kasoro zizlizopo zinazotia hofu katika upatikanaji wa takwimu za kuaminika, kwa wakati muafaka, na fursa ya kuzipata na jambo ambalo linaathiri watoto na familia zao.

Kwa mfano  yamesema orodha ya wakimbizi kulingana na umri zilizopo kwenye shirika la UNHCR ni asilimia 56 tu, huku kukiwa na  asilimia 20 tu ya nchi zilizo na takwimu za wakimbizi wa ndani kwenye maeneo ya migogoro ambazo zimegawanywa kutokana na umri, na robo ya nchi duniani hazina takwimu za wahamiaji  zilizogawanywa kutokana na umri zikiwemo nchi 43 barani Afrika.

Kwa mujibu wa Laurence Chandy mkurugenzi wa idara ya takwimu, utafiti na será wa UNICEF, kukosekana kwa tarifa sahihihi za watoto wahamiaji na wakimbizi wa ndani kunawakosesha watoto hao ulinzi na huduma wanazohitaji.

Pia amesema “pengo hilo kimsingi linaathiri uwezo wa mashirika kama UNICEF kuwasaidia watoto hao kwa sababu hayajui ni kina nani, wako wapi au nini wanahitaji.”

Mashirika hayo yametoa wito kwa nchi kuziba mapengo hayo kwa kuboresha ukusanyaji takwimu na kuimarisha ushirikiano ili kubadilisha takwimu na kuzilinganisha. Inakadiriwa kulikuwa na watoto milioni 28 waliolazimika kutawanywa mwaka 2016, lakini idadi kamili huenda ni kubwa zaidi.

Mashirika hayo la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, la kuhudumia wakimbizi UNHCR, la uhamiaji IOM, Eurostat na shirika la ushirikiano wa kiuchumi kwa maendeleo, OECD katika wito wao wa kuwalinda watoto yamesama ulinzi huo unaanza na takwimu bora na sahihi, na yameonyesha ni jinsi gani takwimu zilivyo muhimu kwa kuelewa mwenendo wa uhamiaji wa kimataifa ili kuweza kuunda sera za kusaidia makundi yaliyo hatarini kama watoto.

Wito huo wa “kuchukua hatua” unathibitisha kasoro zizlizopo zinazotia hofu katika upatikanaji wa takwimu za kuaminika, kwa wakati muafaka, na fursa ya kuzipata na jambo ambalo linaathiri watoto na familia zao.

Kwa mfano  yamesema orodha ya wakimbizi kulingana na umri zilizopo kwenye shirika la UNHCR ni asilimia 56 tu, huku kukiwa na  asilimia 20 tu ya nchi zilizo na takwimu za wakimbizi wa ndani kwenye maeneo ya migogoro ambazo zimegawanywa kutokana na umri, na robo ya nchi duniani hazina takwimu za wahamiaji  zilizogawanywa kutokana na umri zikiwemo nchi 43 barani Afrika.

Mgogoro wa Yemen wananchi wazidi kukumbwa na madhila wakiwemo watoto
PIcha: WHO Yemen
Mgogoro wa Yemen wananchi wazidi kukumbwa na madhila wakiwemo watoto

Kwa mujibu wa Laurence Chandy mkurugenzi wa idara ya takwimu, utafiti na sera wa UNICEF, kukosekana kwa tarifa sahihihi za watoto wahamiaji na wakimbizi wa ndani kunawakosesha watoto hao ulinzi na huduma wanazohitaji.

Pia amesema “pengo hilo kimsingi linaathiri uwezo wa mashirika kama UNICEF kuwasaidia watoto hao kwa sababu hayajui ni kina nani, wako wapi au nini wanahitaji.”

Mashirika hayo yametoa wito kwa nchi kuziba mapengo hayo kwa kuboresha ukusanyaji takwimu na kuimarisha ushirikiano ili kubadilisha takwimu na kuzilinganisha. Inakadiriwa kulikuwa na watoto milioni 28 waliolazimika kutawanywa mwaka 2016, lakini idadi kamili huenda ni kubwa zaidi.

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter