Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa Benki ya Dunia kwa Iraq wafikia dola bilioni 4.7

Familia waathirika wa vita vya ISIS wakimbia wakipita katikati ya mijendo iliyobomolewa na mikombora Al Mamum, karibu na Mosul, Iraq.
UNICEF/Alessio Romenzi
Familia waathirika wa vita vya ISIS wakimbia wakipita katikati ya mijendo iliyobomolewa na mikombora Al Mamum, karibu na Mosul, Iraq.

Msaada wa Benki ya Dunia kwa Iraq wafikia dola bilioni 4.7

Amani na Usalama

Benki ya Dunia na serikali ya Iraq zimetiliana saini makubaliano ya miradi mikubwa miwili yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 510.

Miradi hiyo inalenga kusaidia wairaq kuboresha maisha yao kwa kuimarisha usambazaji wa maji na kuaniza vyanzo vya ajira.

Miradi hiyo miwili pamoja na mwingine  unaoendelea wa kuimarisha operesheni za dharura ukiwa na thamani ya dola milioni 750, itafanya usaidizi wa Benki ya Dunia kwa Iraq kufikia dola bilioni 4.7 ikilinganishwa na dola milioni 600 miaka minne iliyopita.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano hayo kando mwa mkutano wa kimataifa wa kujenga upya Irak huko Kuwait Rais wa benki hiyo Jim Yong Kim amesema kuwa watatumia ujuzi wote walio nao kuwekeza katika Iraq mpya na iliyo na thabiti.

Aidha amesema kuwa watashirkiana bega kwa bega na sekta binafsi ili kuiunga mkono Iraq.

Mbali na msaada wa kifedha Benki ya Dunia, kwa ushirikiano na serikali ya Iraq, imekuwa ikiipiga jeki Iraq kupitia misaada ya kiufundi ili kujikwamua katika shida ilizonazo pamoja na kuweka msingi  wa uwekezaji  katika sekta ya binafsi ya Iraq.