Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msimu wa mafua makali wabisha hodi.

Watu ni lazima waoshe mikono yao kwa maji na  sabuni baada ya kukohoa kama njia moja ya kuzia kusambaa kwa  virusi vya homa kali  aina ya A(H1N1)
UN/makala
Watu ni lazima waoshe mikono yao kwa maji na sabuni baada ya kukohoa kama njia moja ya kuzia kusambaa kwa virusi vya homa kali aina ya A(H1N1)

Msimu wa mafua makali wabisha hodi.

Afya

Msimu wa mafua makali tayari umebidha hodi katika nchi kadhaa huku ukinyemelea mataifa mengine, limesema shirika la afya duniani, WHO.

Kutokana na hali hiyo WHO imetoa mwongozo wa kuzingatia wakati wa msimu huu wa mafua makali ambapo baadhi ya nchi zimepata idadi kubwa zaidi ya wagonjwa.

Nchini Marekani viwango vya wanaokwenda hospitalini kutibiwa mafua  ni sawa na  vile vilivyotokea misimu saba iliyopita.

Maeneo ya tropiki kama vile barani Afrika, taarifa za visa vya mafua zimeripotiwa katika nchi kama vile Madagascar, ilhali  bara la Asia nchi za Pakistan na Singapore ndiyo zinaongoza.

Kwa mantiki hiyo WHO imependekeza nchi ambazo tayari zinakabiliwa na ugonjwa huo kupatia chanjo makundi ambayo yanakabiliwa zaidi na mafua hayo.

WHO inasema njia bora ya kuzuia mafua hayo ni chanjo ambapo hutolewa kabla ya kuanza kwa msimu wa ugonjwa huo na inashauriwa mtu apatiwe chanjo kila mwaka kwa sababu kila mara virusi vya mafua hubadilika.