Wakimbizi wa DRC wazama Ziwani, Uganda

12 Februari 2018

Habari za simanzi kutoka Uganda amabko maelfu ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wanakimbilia kusaka usalama kila uchao zinaonyesha kwamba wakimbizi 4 wa familia moja wamefariki dunia baada ya boti walimokuwa wakisafiria biruka na kuzama katika ziwa Albert. 

Wakimbizi hao watano walikuwa kwenye boti moja wakitoroka mapigano yaliochacha baian ya Walendu na Wahema Jimboni Ituri, hiyo jana.

Mmoja ndiye aliokolewa na wavuvi waliokuwa karibu. Kilichosababisha ajali hiyo bado hakijaelewaka.

Steven John Ekom, Mwenyekiti wa kamati mahsusi  ilioundwa kushughulikia janga hili la wakimbizi wialyani Hoima amesema jeshi na polisi wanamaji wa Uganda wanaendelea kutafuta miili ya wakimbizi hao waliozama wakikaribia ufukwe Sebagoro.

Wiki iliopita, wakimbizi wengine wawili pia waliripotiwa kuzama katika visa tofauti.

Mwaka 2014 wakimbizi Zaidi ya 100 walizama katika Ziwa hilohilo walipokuwa wakirejea DRC, kutoka kambi ya Kyangwali, kiviao.

Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, inasema idadi ya wanaokimbia DRC imeongezeka hadi 569 kutoka 346 katika wiki chache zilizopita.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud