Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu wanaendelea kufungasha virago Ituri, DRC na kumiminika Uganda

Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakikimbia ghasia jimbo la Ituri. Picha: UM

Maelfu wanaendelea kufungasha virago Ituri, DRC na kumiminika Uganda

Amani na Usalama

Shirika la Umoja w aMataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), limeripoti kuwa wakimbizi takribani 4,000 wamekimbilia Uganda kufuatia kushamiri kwa mzozo wa kikabila Jimbo la Ituri na mashambulizi ya vikundi vilivyojihami Jimboni Kivu Kaskazini katika kipindi cha wiki moja tu. 

Msemaji wa UNHCR, Uganda, Roco Nuri, amesema wamesajili wakimbizi 3,977 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya ongo( DRC) kati ya 30 Januari na 5 Februarim waka huu.

Amesema kumiminika kwao kumeibua changamoto lukuki katika utoaji wa huduma ya afya, na mahitaji mengine ya maisngi kama malazi na chakula, ukizingatia kuwa asilimia 54 yao ni watoto.

Manmo tarehe tano Februari pekee, wakimbizi 1386 waliwasili, Uganda wakisafiri kwa mitumbwi hatarishi ikiwemo ile za wavuvi kwenye Ziwa Albert, wakitoroka  mashambulizi ya kikabila baina ya Walendu na Wahema jimboni Ituri.

Idadi ya wanaokimbia vurugu DRC, na kuingia Uganda imeongezeka hadi 569 kwa siku kutoka 346 wiki zilizopita.