Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita dhidi ya ISIL vyaingia awamu mpya:Voronkov

Moja ya mitaa huko Douma, eneo la Ghouta mashariki nchini Syria ambako mapigano yamesambaratisha maeneo ya makazi.
UNICEF/Amer Al Shami
Moja ya mitaa huko Douma, eneo la Ghouta mashariki nchini Syria ambako mapigano yamesambaratisha maeneo ya makazi.

Vita dhidi ya ISIL vyaingia awamu mpya:Voronkov

Hii leo kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wajumbe wameelezwa kuwa ingawa yaonekana kuwa magaidi wa ISIL wamesambaratishwa baadhi ya maeneo, bado kundi hilo ni tishio kwa kuwa limeibuka na mbinu mpya za kusajili wafuasi wanaoweza kufanya mashambulizi ya hapa na pale.

Vita dhidi ya kikundi cha wapiganaji wa ISIL au Da’esh bado ni changamoto duniani na vinahitaji hatua za dharura na za pamoja.

Hayo yemetamkwa na mkuu wa ofisi ya Umoja wa mataifa inayohusika na kukabiliana na ugaidi Vladimir Voronkov wakati akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York,

Marekani kuhusu hali ya ugaidi hususan wa kundi hilo la ISIL kwa sasa.

Bwana Voronkov alikuwa akigusia ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu ISIL ambapo wametaka juhudi za pamoja  katika kufanikisha juhudi zao.

(Sauti ya Vladmir Voronko)

Natoa wito kwa mataifa wanachama kuzidisha juhudi zao kuimarisha ushirika wa kimataifa ili kukabiliana dhidi ya ugaidi na  vitendo vya misimamo mikali na kufikisha mahakamani wanaotenda maovu hayo”.

Bwana Voronkov amesema kwa mujibu wa ripoti ya sita  kuhusu magaidi hao, kazi dhidi ya makundi hayo ni bado .

(Sauti ya Vladmir Voronko)

Vita dhidi ya ISIL vinaingia awamu mpya.Ripoti hii inaonyesha kama licha ya ISIL kupata pigo kijeshi  mwaka jana nchini Iraq, Syria na kusini mwa Ufilipino, bado kundi hilo pamoja na washirika wao  ni tishio  duniani”.

Amegusia mbinu mpya za ISIL akisema kuwa ripoti inaonyesha kuwa ISIL imeachana na mpango wake wa kuteka ardhi na kuwa na maeneo yao na badala yake imeanzisha mfumo wa kuwa na vikundi vidogovidogo vya watu ambao wanaweza kuitwa wanachama damu ambao wanaweza kuendesha mashambulizi ya hapa na pale.

Pia amesema kuwa ripoti inaonyesha kama dawati la propaganda la ISIL linapungua makali japo wanachama wake pamoja na wanaowaunga mkono baado wana uwezo wa kutumia na kuendelea kutumia mitandao ya kijamii kupanga mashambulizi.