Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shirika la skauti na UNEP waafikiana kutoa elimu na kulinda mazingira

Taka zilizopo kando ya bahari. Picha: UM

Shirika la skauti na UNEP waafikiana kutoa elimu na kulinda mazingira

Tabianchi na mazingira

Shirika la muungano wa skauti duniani (WOSM) na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP leo wamedumisha ushirikiano wao kuhusu masuala ya mazingira kwa kutambua changamoto kubwa zinazoikabili dunia hivi sasa na umuhimu wa mchango wa vijana katika kujenga dunia endelevu kandoni mwa jukwaa la kimataifa la miji mjini Kuala Lumpur.

Muafaka huo umekuja wakati pande ote zikiadhimisha miaka 10 tangu kuzinduliwa kwa mpangoa wa kimataifa wa skauti kwa ajili ya mazingira (WSEP) mwaka 2008.

Skauti kote duniani wamekamilisha maelfu ya miradi ya mazingira chini ya usimamizi wa WSEP ikiwemo utunzaji wa matumbawe Indonesia, na kuelimisha kuhusu mabadiliko ya tabia nchi Morocco, na kupata tuzo ya kimataifa ya mazingira.

Katibu Mkuu wa shirika hilo la skauti duniani, Ahmad Alhendawi, na mkurugenzi mtendaji wa UNEP, Erik Solheim, wametia saini muafaka huo wa ushirika kandoni mwa jukwaa la 9 la dunia la masuala ya miji linaloendelea Kuala Lumpur Malaysia.

Miradi mipya ya pamoja itahusiha kusafika mazingira ya bahari kw kusanya taka, upandaji wa mita kutoa elimu ya mazingira kwa vijana na masuala ya tabia nchi.