Tuhuma za matumizi ya silaha za kikemikali zijibiwe vilivyo
Mwakilishi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya upokonyaji silaha Izumi Nakamitsu amesema ushahidi zaidi wa matumizi wa silaha za sumu zilizopigwa marufuku nchini Syria ni sharti zipewe jibu la kutosha na Baraza la Usalama la umoja huo.
Bi. Nakamitsu amesema hayo leo wakati akihutubia Baraza la Usalama kuhusu kazi inayofanywa na Umoja wa Mataifa pamoja na a shirika la pamoja la kupinga matumizi ya silaha za kemikali.
Amesema kuwa uteketezwaji kamili wa vituo vya serikali 27 unapashwa kukamilishwa katika kipindi kijacho cha miezi miwili na kuongeza kuwa kikosi cha OPCW kinachotafuta ukweli -FFM- katika madai ya vikosi vya serikali kutumia silaha za sumu kitawasilisha ripoti yake haraka iwezekanavyo.
Madai mengi yanahusu matumizi ya gesi ya Chlorine. Madai hayo baado yanasikika ikiwemo matumizi yake mwishoni mwa juma lililopita katika mji wa Saraqed.
Taarifa zasema kuwa watu tisa wamehudumiwa wakiwa na matatizo ya kupumua baada ya shambulio la bomu linalodhaniwa lilikuwa na gesi katika eneo la mji wa Idlib linalodhibitiwa na waasi.