Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres atangaza hatua 5 kutokomeza ukatili wa kingono ndani ya UN

Katibu Mkuu wa UM Antonio Guterres
PICHA/UN/Evan Schneider(maktaba)
Katibu Mkuu wa UM Antonio Guterres

Guterres atangaza hatua 5 kutokomeza ukatili wa kingono ndani ya UN

Masuala ya UM

Umoja wa Mataifa umetangaza hatua tano za kukabiliana na ukatili wa kingono dhidi ya wanawake ndani ya chombo hicho kufuatia suala hilo kuanza kupatiwa umakini inavyotakiwa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari hii leo kwenye makao makuu jijini New York, Marekani ametaja hatua hizo ni

(Sauti ya Antonio Guterres)

“Mosi tumeazimia kuchukua kwa umakini tuhuma hizo kwa umakini kabisa, zilizopita na za sasa. Pili wafanyakazi waliokumbwa na ukatili wafahamu wapi pa kupata msaada hivyo tunaanzisha namba ya simu ya msaada ambako watapata msaada kwa siri na itaanza kazi katikati ya februari. Tatu. Nimeanzisha kikosi kazi cha viongozi kutoka Umoja wa Mataifa ili kusaidia kushughulikia usaidizi kwa waathirika.”

Bwana Guterres ametaja hatua ya nne kuwa ni kuwalinda watoa taarifa, akiwakumbusha wafanyakazi jukumu lao la kutoa taarifa ili kusaidia waathirika huku hatua ya tano ikwia ni kufanya utafiti miongoni mwa wafanyakazi wa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ili kupata ukweli kamili.

Katibu Mkuu amesema ingawa mfumo dume ulioota mizizi kwenye serikali, sekta binafsi, mashirika ya kimataifa na yale ya kiraia bado ni kikwazo katika kutokomeza ukatili wa kingono, bado kupitia hatua alizotangaza ujumbe wake ni kwamba..

(Sauti ya Antonio Guterres)

“Hatutavumilia ukatili wa kingono wakati wowote, pahala popote. Na tutaendelea kubadilisha kasi hiyo na kuweka mamlaka zaidi mikononi mwa wanawake kama njia ya kuzuia na kutokomeza ukatili wa kingono na matumizi mabaya ya madaraka kwenye Umoja wa Mataifa.”