Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Diplomasia ya kibinadamu “haiendi popote” nchini Syria.

Jan Egeland akizungumza na wanahabari mjini Geneva, Uswisi. (Picha: UN/Luca Solari)

Diplomasia ya kibinadamu “haiendi popote” nchini Syria.

Msaada wa Kibinadamu

Kwa miezi miwili sasa hakuna msafara wowote wenye misaada ya kibinadamu ambayo imewafikia raia walioko katika maeneo ya Syria yaliyozingirwa.

Akizungumza Alhamisi mjini Geneva, Uswisi, mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, Jan Egeland, amesema kuwa  juhudi za kidiplomasia zaonekana kama kile alichoita ‘kisu butu’ akiongeza kuwa ni sawa na kupoteza maisha ya mamia ya watu.

 

Wananchi wengi wamekuwa wanakimbilia Idlib, ambako mapigano sasa yamepamba moto na  hawana lingine bali kuchanja mbuga kwa mara nyingine tena.

 

Image
Watoto wakiwa mjini Aleppo nchini Syria.(Picha:UNICEF/Romenzi), by dsu-admin

Msafara wa misaada wa hivi karibuni uliwasili huko mji wa al-Nashibiya Novemba 28 mwaka jana na ulikuwa na msaada wa kuwatosheleza tu watu 7,200. 

 

Bw  Egeland amesema kuwa historia ya ya vita vya Syria ni kuwa kwa zaidi ya miaka mitano sasa watu milioni kadhaa wamekuwa  wakikimbia kila mwaka kuokoa maisha yao  na hali sasa inaomba kuwepo kwa ushitishwaji  wa mapigano.