Guterres atiwa hofu na mvutano Sahara Magharibi

Helikopta ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Sahara Magharibi, MINURSO ikiwa kwenye doria. (Picha:Minurso)

Guterres atiwa hofu na mvutano Sahara Magharibi

Katibu Mkuu wa Umoja wa  Mataifa Antonio Guterres ana wasiwasi mkubwa kutokana na kuendelea kuongezeka kwa mvutano kwenye eneo la Guerguerat kusini mwa Sahara Magharibi.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema eneo hilo ambalo kwa mujibu wa makubaliano ni eneo huru, liko katikati mwa mpaka wa Morocco na Mauritania.

Bwana Guterres amesisitiza ya kwamba kitendo cha kikundi cha Polisario Front kujiondoa eneo hilo mwezi Aprili mwaka 2017, halikadhalika askari kutoka Morocco ni muhimu katika kurejea kwa mazungumzo chini ya mjumbe wake Horst Kohler.

Ametoa wito kwa pande mbili hizo kujizuia na kuepuka mvutano zaidi huku akitaka eneo hilo huru lisiwekewe vizuizi vyovyote vitakavyoathiri misafara ya kiraia na kibiashara.