Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajawazito Aleppo wapata ahueni

Kituo cha afya ya uzazi zcha muda katika eno la Sheikh Maqsoud mjini Aleppo, nchini Syria. Picha: UNFPA

Wajawazito Aleppo wapata ahueni

Hatimaye timu mbili za wahudumu wa afya ya uzazi zimefika kwenye eno la Sheikh Maqsoud mjini Aleppo, nchini Syria , eneo ambalo halijafikika kwa kipindi kirefu katika miaka saba ya mapigano na hivyo kuzorotesha kabisa utoaji wa huduma ya afya. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya John Kibego)
Timu hizo ni kutoka shirika la Umoja wa Matifa la Idadi ya watu, UNFPA, likishirikiana na shirika la msalaba mwekundu nchini Syria tarehe 28 Disemba ikiwa ni mara ya kuanza shirika la Umoja wa Mataifa kuingiza msaada katika eno hilo la Sheikh Maqsoud.
Watu zaidi ya 65,000, wengi wao wakiwa ni watoto, wanawake na wazee wanahitaji msaada wa kibinadamu, huku idadi ikitarajiwa kuongezeka sanjari na idadi a wanaorejea makwao.
Kuna kituo kimoja cha afya pekee kinachohudumia watu wapatao  50 kwa siku, ambacho hakikidhi mahitaji ya huduma ya afya katika eneo hilo ambako wanawake karibu 3,000 ni wajawazito.
Mwakilishi wa UNPFA, Syria, Massimo Diana, amesema mzoozo hutia hatarini akinamama na watoto wachanga kwani matatizo ya kimwili na kisaikolojia husababisha matatizo wakati wa kujifungua.
Hata hivyo ametoa matumaini akisema UNFPA, Syria, inaendelea na mipango ya kupeleka mahitaji ya dharura pamoja na vifaa vya kuhakikisha usalama wakati wa kujifungua.