Hatua za wanawake India zashangaza wengi

2 Januari 2018

Ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 inatoa kipaumbele katika suala la ujasiriamali ikiwa ni njia mojawapo ya kutokomeza umasikini.

Umoja wa Mataifa na washirika wake wamekuwa mstari wa mbele  katika kutoa elimu na pia fursa kwa asasi za kiraia, serikali  mbalimbali duniani na pia mashirika binafsi  ili kuimarisha ujasiriamali.

Wanawake nao kupitia mafunzo hayo hawajabaki nyuma bali wako mstari wa mbele kutumia fursa hizo za biashara katika kujiendeleza. Leo tunaelekea nchini India katika vijiji vya Bihar ambako wananawake 12 wamekuwa nguzo na pia mfano wa kuigwa, baada ya kuanzisha kampuni yenye mafanikio  kwa msaada wa Benki ya dunia. Je wamefanya nini? Patrick Newman anafafanua katika makala ifuatayo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud