Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sanaa ya uchoraji yafaa kutimiza SDGS: Balozi Kamau

Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili
Msanii Kenneth Malomba kutoka Malawi.

Sanaa ya uchoraji yafaa kutimiza SDGS: Balozi Kamau

Mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa, Balozi Macharia Kamau amesema vijana wanaweza kutumia sanaa kuinua kipato na kufanikisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Katika mahojiano na idhaa ya Kiswahili mjini New York, Marekani wakati akihudhuria maonesho ya uchoraji yalioandaliwa na kijana Kenneth Malomba kutoka Malawi, Balozi Kamau amesema mbinu ya uchoraji ni muhimu kwani inaweza kukomboa vijana na jamii akiongeza kuwa..

( Sauti ya Balozi Macharia Kamau)

image
Michoro iliyoandaliwa na Msanii Kenneth Malomba kutoka Malawi. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili
Kwa upande wake msanii Malomba amesema vijana barani Afrika wana kila sababu ya kutumia Sanaa hiyo kwani.

( Sauti Kenneth Malomba)

"Nawashauri kwamba watumie sanaa kufikisha ujumbe. Ni moja ya zana bora ya kufikisha ujumbe. Uzuri wake ni kwamba wakati unafikisha ujumbe watu huburudika."

image
Michoro iliyoandaliwa na Msanii Kenneth Malomba kutoka Malawi. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili