Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CAR hali bado ni tete kwa wanaohitaji msaada haraka:OCHA

Picha: UNICEF
Mtoto nchini CAR apimwa katika juhudi za kuthibiti utapiamlo.

CAR hali bado ni tete kwa wanaohitaji msaada haraka:OCHA

Hali ya takribani watu 100,000, wakiwemo wakimbizi wa ndani na jamii zinayowahifadhi mjini Paoua nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR bado ni tete.

Kwa mujibu wa matokeo ya tathimini iliyofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA na wizara ya masuala ya kibinadamu ya serikali ya CAR juma hili,  wakimbizi wa ndani 60,000 na wenyeji 40,000 wa mji wa Paoua wanahitaji msaada wa dharura ili kuokoa maisha yao.

Hofu ya kiafya inaongezeka huku kukiwa na tarifa za maiti kutupwa kwenye visima au kutelekezwa barabarani vijijini na kutishia maambukizi ya magonjwa.

Tathimini hiyo inasema waathirika wakubwa ni watoto na wanawake ambao miongoni mwao 100 ni wajawazito jambo linaloongeza hofu ya usalama pia.

Wakimbizi hao wa ndani wanaishi katika mazingira duni na visa vingi vya ukatili wa kijinsi vimekuwa vikiripotiwa. Najat Rochdi ambye ni mratibu wa OCHA nchini CAR anasema ingawa msaada wa afya, ulinzi na chakula unatolewa lakini hautoshelezi. Na wakimbizi hao sasa hawataki tena kukaa kambini na kwamba

(SAUTI YA NAJAT ROCHDI)

“Msimamo wao uko dhahiri wanataka kurejea vijijini kwao haraka iwezekanavyo, na kitu cha kwanza cha msingi ni kuwa na usalama na MINUSCAR imetoa muda maalumu kwa makundi ya waasi ikiwataka waondoke katika eneo hilo ikiwemo katika vijiji wanakoingia wakimbizi wa ndani. Na wamepewa saa 48 na punde hilo litakapotekelezwa itakuwa rahisi sisi kuwasindikiza na kusaidia kurejea hadi katika vijiji walikotoka.”Kikosi cha jeshi la India kilichoko  mkoa wa Malakal Sudan Kusini, kama sehemu ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kimetoa msaada wakutibu mifugo ya wafugaji wa eneo la Akola,lililoko umbali wa kilomita sitini na tano, kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa jimbo hilo.