Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wasaidia wakulima kudhibiti panya Mtwara, Tanzania

Wakulima huko wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara wakifuatilia mafunzo shambani kuhusu kilimo kinachohimili mabadilko ya tabianchi. (Picha:Videocapture)

Wataalamu wasaidia wakulima kudhibiti panya Mtwara, Tanzania

Nchini Tanzania serikali inaendelea na jitihada za kusaidia wakulima ili waweze kuzingatia mwongozo wa kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi na hatimaye kujiongezea kipato na kuwa na uhakika wa chakula.

Mwongozo huo uliandaliwa na shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania ambao hata hivyo bado panya wamekuwa kikwazo kwa utekelezaji wa mwongozo huo.

Mathalani huko wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara, wakulima wanajitahidi kupanda mahindi kwa ajili ya lishe na kuuzwa kwa ajili ya kipato lakini bado panya wanafukua mbegu.

Akihojiwa na Idhaa hii kutoka Nanyumbu, mtaalamu wa zana za kilimo wilaya humo, Benedict Makombe amesema..

image
Mkulima kwenye shamba ambalo limewekwa sumu na panya sasa hawawezi kuharibu mazao. (Picha:Kwa hisani ya Afisa zana-Nyanyumbu)
(Sauti ya Benedict Makombe)

Ili kukabiliana na panya, Bwana Makombe amesema wananchi huandaa chambo ya panya ambayo huchanganywa na sumu kutoka kituo cha udhibiti wa panya na kwamba...

(Sauti ya Benedict Makombe)