Skip to main content

Raia wa DRC waendelea kufungasha virago na kukimbilia nchi jirani

Wakimbizi nchini DRC. Picha: © UNHCR/M.Brook

Raia wa DRC waendelea kufungasha virago na kukimbilia nchi jirani

Maelfu a raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wanedelea kufungasha virago na kukimbilia nchi jirani za Burundi, Tanzania na Uganda katika kiwango cha kutia hofu limesema leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Siraj Kalyano na taarifa kamili.

(TAARIFA YA SIRAJ)

Kwa mujibu wa shirika hilo maelfu ya wanawake, watoto na wanaume wamezihama nyumba zao na kuacha kila kitu kufuatia kuchachamaa kwa operesheni za kijeshi zinazoendeshwa na wanamgambo wa Mai Mai katika jimbo la kivu Kusini. Tangu wiki iliyopita watu takribani 7,000 wameingia Burundi, wengine 1200 wameingia Tanzania na inaaminika maelfu wengine wametawanywa ndani ya Kivu Kusini wakiishi katika mazingira magumu bila malazi wala chakula. Babar Baloch ni msemaji wa UNHCR Geneva

(SAUTI YA BABAR BALOCH)

“Wakimbizi tuliozungumza nao wanasema wamekimbia kuingizwa kwa shuruti jeshini, vita na ukatili mwingine unaofanywa na makundi yenye silaha, huku wengine wakisema wamekimbia operesheni za kijeshi na kutokana na hofu. Ni muhimu sana watu wanaokimbia kuruhusiwa kufanya hivyo kwa usalama na kwamba fursa ya misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi wa ndani iwezeshwe.”

Ameongeza kuwa waathirika sio raia wa Congo peke yake bali pia kuna wakimbizi 43,000 wa Burundi walioko upande wa pili wa ziwa Kivu jimboni humo hasa kwenye maeneo ya Lusenda na Mulongwe.