Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hema linalohimili mabadiliko ya tabia nchi ni nuru kwa wakimbizi Uganda

Hema maalumu linalohimili mabadiliko ya tabia nchi, Uganda. Picha: James Makumbi

Hema linalohimili mabadiliko ya tabia nchi ni nuru kwa wakimbizi Uganda

Tabianchi na mazingira

Huko Uganda, wabunifu wameibuka na hema jipya linalohimili mabadiliko ya tabianchi. 

Wakimbizi wa Sudani Kusini waishio kwenye makazi ya wakimbizi ya Maaji -Adjuman kaskazini mwa Uganda sasa wananeemeka na huduma ya afya kupitia hema maalumu linalohimili mabadiliko ya tabia nchi. Hema hilo la aina yake duniani limetolewa kama zawadi kwa wakimbizi hao na wanafunzi wa chuo kikuu cha Makerere baada ya hema hilo kuwawezesha kushinda tuzo ya ubunifu wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Kwa maelezo zaidi tuungane na Siraj kalyango