OCHA yaipatia Ethiopia dola milioni 10 kukwamua wenye shida zaidi

29 Januari 2018

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya dharura, OCHA imetangaza dola milioni 10 kwa ajili ya usaidizi wa watu walio hatarini zaidi Ethiopia.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya dharura, OCHA imetangaza dola milioni 10 kwa ajili ya usaidizi wa watu walio hatarini zaidi Ethiopia.

Mkuu wa OCHA Mark Lowcock amesema fedha hizo zinatoka mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa, CERF, na kwamba wametoa fedha hizo baada ya kutembela vituo vya wakimbizi wa ndani ambako wameshuhudia jinsi watu walivyo na mahitaji makubwa kama ilivyoombwa na serikali ya Ethiopia.

Wakimbizi hao wa ndani wanatokana na mzozo unaoendelea kati ya wakazi walio mpakani wa maeneo ya Oromia na Somali nchini Ethiopia, mzozo ulioanza mwaka jana.

Kwa mantiki hiyo fedha hizo za CERF zitasaidia juhudi za serikali na wadau wa misaada za kutoa misaada ya kuokoa maisha ikiwemo makazim, maji safi na salama na huduma za kujisafi.

Miongoni mwa juhudi za serikali ya Ethiopia ni mradi wa kuwezesha jamii kujikwamua ambapo Bwana Lowcock amesema katika ziara yao nchini humo..

(Sauti  ya Mark Lowcock)

“Tunajaribu kuangalia jinsi tatizo la kibinadamu linavyoongezeka na kupanuka hivi sasa, na pia suluhu zinazoweza kuchukuliwa ambamo kwazo wasaidizi wa kibinadamu na wadau wao watashirikiana kwa karibu kutatua hali ya sasa lakini pia kupata suluhisho la kudumu. Ethiopia ni nchi ambayo imeweza kupunguza hatari ya wananchi kutumbukia kwenye njaa katika maeneo mengi kupitia mpango wake wa kuwezesha kaya maskini vijijini, Tunachosikia kutoka kwa serikali na wananchi ni jinsi gani ya kuborsha mpango huo ili utumike katika maeneo haya yenye ukame.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter