Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlo baado ni shida katika maeneo ya migogoro duniani

Eneo lilolochomwa na ufyatuliaji wa risasi kufuatia uvamizi wa ng'ombe nchini Sudan Kusini. Picha: FAO

Mlo baado ni shida katika maeneo ya migogoro duniani

Msaada wa Kibinadamu

Ripoti mpya ya pamoja ya mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lila la chakula na kilimo FAO na la mpango wa chakula WFP inasema kuwa idadi ya watu walio na njaa duniani imepanda kwa kiasi cha watu millioni 38 kati ya mwaka wa  2015 na 2016. Selina Jerobon na ripoti kamili.

(Taarifa ya Selina Jerobon)

Mashirika hayo yanasema idadi ya wenye njaa mwaka 2015 ilikuwa millioni 777 lakini kutokana na shida na machafuko, mwaka uliofuatia wa 2016 idadi iliongezeka hadi millioni 815.

Idadi kubwa ya wenye njaa wanaishi katika mataifa yaliyoharibiwa na migogoro.

FAO na WFP wanasema chakula katika mataifa yaliyogubikwa na migogoro kinazidi kupungua , hii ikimaanisha kuwa juhudi za kutoa misaada ya kibinadamu kwa jamii athirika baado ni nyeti mno.

Mataifa yaliyotajwa kuathirika zaidi na njaa ni 16 yakiwemo barani Asia, Afrika , ghuba la uajemi na  Haiti.

Mataifa nane duniani yametajwa kama zaidi ya robo ya raia wake wanakabiliwa na shida ya njaa.

Barani Afrika taifa lililochomoza zaidi ni Sudan Kusini ambako takribani nusu ya raia wake wanakabiliwa na njaa, ikifuatiwa na Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR.

Kati ya yote Yemen ndio inashika bendera kwa kuwa idadi kubwa ya wanaothirika ikiwa ni millioni 17 ya watu ambao ni sawa na asilimia 60.

Ripoti inasema kuwa migogoro ndiyo imekuwa chachu ya kuwepo kwa njaa duniani na kuongeza kuwa kuwepo kwa chakula ni muhimu katika kuleta amani.