Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katu hatutokubali utumwa urejee Afrika- Guterres

Katika Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati akihutubia kikao cha 30 cha Muungano wa Afrika, AU huko Addis Ababa, Ethiopia hii leo. (Picha: Twitter ya msemaji wa UN

Katu hatutokubali utumwa urejee Afrika- Guterres

Haki za binadamu

Mkutano wa kawaida wa 30 wa viongozi wa Afrika ukiendelea huko Addis Ababa, Ethiopia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaja mambo matano ya kuimarisha ushirikiano kati a pande mbili hizo.

Mkutano wa kawaida wa 30 wa viongozi wa Afrika ukiendelea huko Addis Ababa, Ethiopia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaja mambo matano ya kuimarisha ushirikiano kati a pande mbili hizo.

Akihutubia wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Bwana Guterres ametaja mambo hayo kuwa ni amani na usalama, uhamiaji, maendeleo endelevu, mabadiliko ya tabianchi na vita dhidi ya rushwa.

Akizungumzia  uhamiaji,  Katibu Mkuu amerejelea masikitiko yake kuhusu utumwa wa kisasa wakati huu ambapo visa vya utumwa vimeripotiwa huko Libya hivyo amesema..

(Sauti ya Antonio Guterres)

“Utumwa umesababisha madhara makubwa sana kwa Afrika siku zilizopita kwa sisi kukubali aina mpya ya utumwa hii leo. Ni lazima tujinufaishe kwa kiasi kikubwa na faida za uhamiaji ulio salama huku tukitokomeza ukatili na fikra potofu.”

image
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, (wa tatu kushoto) akiwa katika moja ya vikao na viongozi wa Afrika. (Picha:Twitter ya msemaji wa UM)
Hata hivyo amesema hilo litawezekana iwapo kuna fursa zaidi zinazotambulika kisheria ambazo zitawekwa bayana kati ya nchi ambako wahamiaji wanatoka na nchi wanamohamia.

Kuhusu vita dhidi ya rushwa hoja ambayo bara la Afrika imetangazwa mwaka 2018 kuwa mwaka wa kupiga vita rushwa Bwana Guterres amesema rushwa huchochea  usafirishaji haramu wa binadamu, madawa ya kulevya na hata kuondoa imani ya wananchi kwa serikali zao huku ikihatarisha amani na usalama.

(Sauti ya Antonio Guterres)

“Yakadiriwa kuwa katika kila dola moja inayoelekezwa kwenye misaada ya maendeleo, dola moja inapotea kupitia rushwa. Madhara  yake ni makubwa mno na yanakithiri. Umoja wa Mataifa unashirikiana na tume za kitaifa za kutokomeza rushwa ili kumaliza ukwepaji sheria na wahusika wafikishwe mbele ya sheria.Kwa pamoja tunaweza kumaliza kitisho hiki na kuhakikisha kila fedha ya umma na uwekezaji vinaelekezwa pale ambako vinahitajika zaidi na wananchi.”

image
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kulia) akizungumza na Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi "Farmajo" Mohamed, kando mwa vikao vya AU huko Addis Ababa Ethiopia. (Picha:Twitter ya msemaji wa UM)