Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlinda amani kutoka Pakistani auawa DRC

Walinda amani kutoka Pakistani wakiwa kwenye doria Uvira, DRC. (Picha:MONUSCO)

Mlinda amani kutoka Pakistani auawa DRC

Amani na Usalama

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC mlinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO, kutoka Pakistan ameuawa hii leo katika shambulio huko jimbo la Kivu Kusini.

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC mlinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO, kutoka Pakistan ameuawa hii leo katika shambulio huko jimbo la Kivu Kusini.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema katika shambulio hilo huko Lulimmba, kilometa 96 kusini-magharibi mwa Baraka, mlinda amani mwingine alijeruhiwa.

Kufuatia tukio hilo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali huku akituma rambirambi kwa serikali ya Pakistani na wananchi wake na kuwatakia ahueni majeruhi.

Ametaka wahusika wa shambulio hilo wafikishwe mbele ya sheria huku akisisitiza wito wake kwa vikundi vilivyojihami DRC kusalimisha silaha na kusaka suluhu ya malalamiko yao kwa njia ya amani.

Bwana Guterres amesisitiza utayari wa MONUSCO na Umoja wa Mataifa katika kuendelea kufanya kazi na mamlaka za DRC ili kusaidia kushughulikia changamoto za kiusalama nchini humo.