Imani potofu kikwazo cha vita dhidi ya Ukoma- UN

26 Januari 2018

Imani potofu kama vile kulogwa zimeripotiwa kuwa ni kikwazo katika kutibu ugonjwa wa Ukoma wakati huu ambapo visa vipya 200,000 vya ukoma huripotiwa kila mwaka. Ni kutokana na hali hiyo katika maadhimisho  ya siku ya Ukoma duniani tarehe 28 mwezi huu, Umoja wa Mataifa unataka hatua zichukuliwe na serikali zihakikishe zinatokomeza unyanyapaa dhidi ya wagonjwa. Taarifa zaidi na John Kibego.

(Taarifa ya John Kibego)

Huyu ni Rowin Luvanda, mtanzania ambaye ni mgonjwa wa Ukoma, ugonjwa unaoenezwa na vimelea kwa njia ya hewa lakini kwa miaka mitatu alisaka tiba hadi za kienyeji ambako alielezwa kuwa..

(Sauti ya Rowin)

Umoja wa Mataifa umetaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 22 ambamo kila mwaka kuna visa vipya vya wagonjwa ambapo Rowin baada ya kuhangaika miaka 3 hatimaye alikwenda hospitali ya Lugalo jijini Dar es salaam.

(Sauti ya Rowin)

Kufuatia mahangaiko ya Rowin hadi kupata huduma sahihi baada ya miaka mitatu, tumemuuliza  Meneja wa mpango wa Taifa wa kutokomeza Kifua Kikuu na Ukoma nchini Tanzania Dkt. Beatrice Mutayoba je tiba ya ukoma inapatikana wapi?

(Sauti ya Dkt. Mutayoba)

Nchini Tanzania visa vipya ya ukoma bado vinaripotiwa Lindi, Rukwa, Mtwara, Morogoro, Pwani; Tanga, Geita, Dodoma, Tabora na Kigoma.

Ujumbe wa mwaka huu wa siku ya ukoma duniani ni “Tokomeza ukoma kuzuia ulemavu miongoni mwa vijana wetu”.  

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud