Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa yenye maendeleo duni kumudu intaneti 2020:ITU

Cosmas Zavazava, Mkuu wa idara ya msaada wa miradi na usimamizi wa elimu kwenye shirika la ITU.Picha na: Daniel Woldu/ ITU

Mataifa yenye maendeleo duni kumudu intaneti 2020:ITU

Mataifa yenye maendeleo duni zaidi duniani yako mbioni kumudu kuwa na mtandao wa mawasiliano ya intaneti ifikapo mwaka 2020 kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo. Ripoti hiyo iliyotolewa na muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU inasema nchi zenye maendeleo duni au LDC’s zinapiga hatua kubwa katika kufikia fursa ya habari na teknolojia ya mawasiliano.

Nchi zote 47 zimezindua huduma ya mawasiliano ya simu ya 3G na asilimia 60 ya watu wake sasa wako katikia mtandao huo. Kwa mujibu wa Dr. Cosmas Zavazava, mkuu wa idara ya miradi na usimamizi wa elimu wa ITU, baadhi ya nchi za LDCs hivi karibuni zimepanda daraja na kuingia katika orodha ya nchi zinazoendelea, na kuna uhusiano mkubwa vaina ya  maendeleo ya nchi hizo na fursa ya mtandao wa intaneti.

Amesisitiza kuwa ili kusonga zaidi na kufikia lengo la kuwa na mawasiliano ya mtandao kwa wote mwaka 2020 lazima huduma hiyo iwe na gharama nafuu. Hata hivyo ameongeza kuna changamoto mfano

(ZAVAZAVA CUT 1)

“Upatikanaji wa uwekezaji inaweza kuwa kikwazo, kodi katika vifaa vya mawasiliano na nchi nyingi za LDCs zina watu ambao wametawanyika  wengi wako vijijini katika maeneo ambayo ni vigumu kufikika lakini pia tuna nchi zinazojumuisha nchi zijulikanazo kama za visiwa vidogo zinazoendelea na kufikisha huduma huko inakuwa gharama kubwa kwa serikali kuweza kumudu.”

Na kwa hmantiki hiyo

(ZAVAZAVA CUT 2)

“Tunaiweka teknolojia kama njia ya kufikia maendeleo, hivyo tunaangalia ni jinsi gani inaweza kusaidia kufikia malengo ya maendeleo endelevu katika sekta zingine zote. Na pindi hilo litakapojumuishwa katika mipango ya maendeleo ya kitaifa inamaanisha kila sekta itakuwa na bajeti kwa ajili hiyo na kwa kufanya hivyo tutakuwa tunafikia jamii zote na watu watakuwa katika teknolojia.”

ITU inashiriki kwenye kongamano la uchumi la Dunia huko Davos wiki hii ikichgiza umuhimu wa kukumbatia teknolojia kwa ajili ya maendeleo.