Kufurumusha waandamanaji si suluhu ya mzozo wa kisiasa- UN

23 Januari 2018

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kusambaratisha waandamanaji si njia sahihi ya kumaliza mzozo, badala yake inachochea zaidi. John Kibego na maelezo zaidi.,

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kusambaratisha waandamanaji si njia sahihi ya kumaliza mzozo, badala yake inachochea zaidi. John Kibego na maelezo zaidi.,

(Taarifa ya  John Kibego)

Kauli ya ofisi hiyo imetolewa kufuatia hatua ya vikosi vya usalama huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupambana na waandamanaji siku ya Jumapili na kusababisha vifo vya watu 6, majeruhi 68 huku wengine zaidi ya 121 wakisalia korokoroni.

Msemaji wa Ofisi hiyo Ravina Shamdasani amesema wanalaani kitendo hicho ambacho pia kimesababisha kujeruhiwa kwa afisa mmoja wa ofisi hiyo ya haki za binadamu huku magari matatu ya doria ya Umoja wa Mataifa yakishambuliwa. Halikadhalika mabomu ya kutoa machozi yalielekezwa maeneo ya makanisa huko Kinshasa, Goma, Kisangani, Lubumbashi na Bukavu.

Ama hiyo haitoshi..

(Sauti ya Ravina Shamdasani)

 “Nchini kote, huduma za intaneti na ujumbe mfupi au SMS zimetisishwa tangu usiku wa kuamkia jumamosi ya tarehe 20 , ikifuatiwa na kitendo kama hicho cha kusitishwa kwa huduma hizo kwa saa 48 wakati wa maandamano ya tarehe 31 mwezi uliopita.”

Kwa mantiki hiyo Bi. Shamdasani amesema..

(Sauti ya Ravina Shamdasani)

“Kitendo cha kutumia nguvu kusambaratisha waandamanaji hakitatatua mvutano wa kisiasa badala yake kitaongeza. Tunatoa wio kwa mamlaka kushirikiana vyema na wapinzani wa kisiasa, viongozi wa kidini na mashirika ya kirai kuhakiksiha haki za wakongo wote za kushiriki kwenye masuala ya umma yanayohusu nchi yao zinazingatiwa.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter