Kampeni ya “utu hauna gharama” yazinduliwa:UNRWA

22 Januari 2018

Kampeni kubwa ya kuchangisha fedha kwa ajili ya wakimbizi wa kipalestina imezunguliwa leo mjini Gaza na shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA. Tupate tarifa zaidi na Flora Nducha.

Kampeni kubwa ya kuchangisha fedha kwa ajili ya wakimbizi wa kipalestina imezunguliwa leo mjini Gaza na shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA. Tupate tarifa zaidi na Flora Nducha.

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Kampeni hiyo ya kimataifa iliyopewa jina “Utu hauna gharama” imezinduliwa na mkuu wa UNRWA Pierre Krähenbühl kwenye shule ya awali ya wasicha ya Rimal mjini Gaza kwa lengo la kuchangisha dola milioni 500, ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi wa Kipalestina walioko Gaza na kwingineko.

Bwana Krähenbühl ameeleza ni kwa nini kampeni hiyo ni muhimu

( sauti ya Krähenbühl)

“Nawaambia wakimbizi wa Kipalestina hapa Ukanda wa Gaza kwenye ukingo wa Magharibi na Jerusalemu Mashariki , Jordan, Lebanon na mpaka Syria  UNRWA inasimama kama shahidi wa historia ya madhila yenu, tunasimamia haki zen una utu wenu.”

Ameongeza kubwa licha ya kujali yanayowakabili Wapalestina miaka nenda miaka rudi sababu kubwa  kubwa ya uzinduzi wa kampeni hiyo ni

(Sauti ya Krähenbühl)

“kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kwa fedha za ufadhili wa Marekani kwa UNRWA ambako kumeliacha shirika letu na hali ya dharura isiyotarajiwa . Uamuzi huo ulikuwa wa ghafla na wa kuathiri.” 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter