Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa ajira na nakisi ya kazi bora kusalia juu 2018: ILO

Picha na ILO/Peder Sterll
Ajuza kama huyo awa mkimbizi karibu tangu una wake .Ni mkimbizi wa Rohingya kutoka Myanmar.Picha na ILO/Peder Sterll

Ukosefu wa ajira na nakisi ya kazi bora kusalia juu 2018: ILO

Shirika la kazi duniani ILO limetoa ripoti mpya kuhusu hali ya ajira   pamoja na viwango vya kazi bora duniani vilivyoko kwa sasa. Ripoti hiyo inatoa taswira inayoonyesha kiwango cha ukosefu wa ajira duniani kikianza kutengamaa. Lakini kwa upande mwingine  nakisi ya ukosefu wa ajira pamoja na kazi bora itaendelea kusalia juu katika sehemu nyingi duniani.

Ripoti hiyo kwa jina Ajira duniani na mwelekeo wa kijamii wa mwaka 2018,  inasema kiwango cha ukosefu wa ajira duniani kimekuwa kikitengamaa baada ya ongezeko kubwa mwaka 2016. Kiwango kilitarajiwa kufikia asilimia 5.6 mwaka 2017 huku idadi ya wasiokuwa na ajira kuwa zaidi ya millioni 192.

Kutokana na mtazamo wa  kiuchumi duniani unabaki kuwa wa wastani licha ya kuwa  wenye nguvu zaidi kinyume na ukuaji uliotarajiwa 2017 , ripoti inasema kuwa  kichocheo cha ukuaji kati ya 2017 na 2018 ni kazi nzuri ya uwepo wa ajira katika mataifa yaliyoendelea ambapo kiwango cha ukosefu wa ajira kinatabiriwa  kushuka  na asilimia zingine 0.2 mwaka 2018 hadi asili mia 5.5, ambacho ni chini ya cha kabla ya mdororo wa uchumi. Kwa upande mwingine, ukuaji wa ajira unatarajiwa  kushuka licha ya ukuaji wa nguvukazi katika mataifa yanayochipukia. Hata hivyo ukuaji huo umekuwa bora ikilinganishwa na mwaka wa 2016.

Akitoa kauli yake kuhusu ripoti hiyo,Mkurugenzi mtendaji wa ILO, Guy Ryder, amesema  japokuwa ukosefu wa ajira duniani umetengamaa na ukosefu wa kazi nzuri baado umetanda, uchumi wa dunia haujaunda ajira ya kutosha hivyo juhudi za ziada ni lazima zifanywe ili kuboresha viwango vya kazi kwa walionazo na kuhakikisha kuwa faida za ukuaji zinagawanywa sawa.

Na kwa upande wa Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara Ripoti inasema kiwango cha ukosefu wa ajira kinatarajiwa kufikia asilimia 7.2 ambapo hakuna mabadiliko makubwa.Huku mfanyakazi mmoja kati ya watatatu anaishi katika umasikini uliokithiri.